Alhamisi, 8 Machi 2018

Hii ndiyo njia rahisi ya kumuingizia kipato mtu yeyote asiye na mtaji

mafunzo ya ujasiriamali JINSI YA KUANZISHA BIASHARA BILA FEDHA AU KWA MTAJI MDOGO Habari za wakati kama huu mjasiriamali uliyemaanisha, Mimi Mwalimu KAMWELA fanaka na niko tayari kukuletea somo ambalo ni JINSI YA KUANZA BIASHARA BILA MTAJI AU KWA PESA KIDOGO, Niseme hivi inawezekana uko kwenye kundi hili na uko kwenye mazingira magumu yaani huna kipato kinachoeleweka au huna kazi au umesimamishwa kazi labda biashara yako imeanguka, au ulikuwa unadaiwa sana kiasi kwamba benki imekufilisi ama inawezekana tu mambo yameenda kombo sana kwako na inawezekana kabisa umeanza kukata tamaa, lakini nataka baada ya kusikia somo hili la leo uanze kunyanyuka tena, Hivyo tutazungumzia mbinu kadhaa wa kadhaa zitakazokuwezesha wewe kuanza pasipo na chochote kile. 1.KIPAJI ULICHONACHO Tatizo kubwa humu ulimwenguni watu wengi wanadharau vipaji walivyo navyo, leo hii isingekuwa kipaji cha uchoraji tusingemfahamu Masoud Kipanya. Jambo la msingi ni kugundua kipaji ulichonacho na na jambo la pili ni kujiuliza je nawezaje kugeuza hiki kipaji changu kikawa fedha? , Wote tunamfahamu Masanja mkandamizaji, mimi nilipata nafasi ya kumsikiliza akitoa historia ya maisha yake, yeye alisema wakati anakuja Dar alidhani njia pekee ya kuwa tajiri ni kuwa mwanamuziki maana alimuona Mr Blue mtaani kwao anaimba muziki na amefanikiwa kwa hiyo akadhani njia pekee ya kufanikiwa ni kuwa mwanamuziki lakini alipogundua yeye ni Comedian alifuata uwezo ule na mpaka sasa kila mtu anamfahamu Masanja ni nani. Swali la msingi ni je wewe una kipaji gani? swali la pili kwa nini umekua unakidharau kipaji chako? swali la tatu Je utafanya nini kuweza kutumia kipaji chako na kuweza kuanza bila kitu? ukishakuwa na kipaji mara nyingi huitaji kitu chochote kile wewe mwenyewe ndio biashara unachotakiwa ni kutafuta watu na kuanza kuwahudumia halafu mambo ya ofisi yatajileta . Usiilaumu Serikali wala Mungu. 2.UZOEFU Jambo la pili ni uzoefu. Inawezekana ukahamasika na masomo ya hapa darasani lakini usikubali mtaji iwe ni kikwazo. Miaka ya nyuma iliyopita kaka yangu mmoja anayeitwa steven, alihamasika sana na haya mafunzo ya ujasiriamali.Akaandika huu ujumbe ufuatao: “Nimehamasika na haya masomo lakini sina mtaji je nifanye nini? nikamuuliza “Kwani unashughulika na nini?” akasema ”mimi ni mwalimu tu” nikamwambia kwa nini usianzishe shule yako? akasema mimi sina mtaji” nikamwakambia ”Je nyumbani kwako huna sebule? ” akasema ”ninayo” nikamwambia ”anzia hapo sebuleni kwako” akaanza pale sebuleni kwake baadae akajenga darasa la mabati na akaendelea na kuendelea na sasa hiv steven ana shule kubwa jijini mbeya.Je una uzoefu gani! je wewe nimtu wa computer kwa nini usianzishe ofisi yako? je wewe ni makenika kwa nini usifungue gereji yako? na wewe mwana MALENGO VIP CLASS je una uzoefu gani? Tumia uzoefu wako ulionao kujiingizia kipato. 3. UWEZO ULIOJIJENGEA Aina ya tatu ya jinsi kuanza biashara bila kitu ni Uwezo binafsi uliojijengea kwa kipindi fulani, Nitatoa mfano wa mimi mwenyewe, namshukuru Mungu kwa uwezo niliojijengea wa kuweza kusoma na kuandika vitabu. Miaka kadhaa wakati najiuliza nifanye biashara gani, niingie kwenye ujasiriamali kwa staili ipi? siku moja ndio nikapata majibu kuwa watu wengi sana huwa wakizungumza na mimi katika semina huwa wanaishia kuniuliza hivi wewe umesoma wapi? au wewe umeishi wapi? mbona unafundisha kwa namna hii? Pale ndio nilipopata majibu kuwa mimi natakiwa niwafundishe watu wengine. Je wewe umejijengea uwezo gani na utaugeza vipi uweni biashara yako? 4.ELIMU ULIYO NAYO Kuna tofauti kati ya elimu uliyonayo na uwezo uliojijengea, hapa tunaongelea zaidi ile elimu rasmi ya madarasa labda una degree fulani jinsi ambavyo unaweza kubadili ile elimu na ukajiajiri, sio lazima ukaajiriwa unaweza kujiajiri kwa elimu hiyo hiyo uliyo nayo, nafahamu watu wengi ambao wamesoma na hawajahi kuajiriwa kabisa mfano Paul Mashauri yeye anaandika vitu vizuri kwenye mitandao mbalimbali vya ujasiriamali anahamasisha wengine lakini hajawahi kuajiriwa na mtu yoyote yule au na shirika lolote lile kwa sababu ya kuelewa haya mambo.Je unaitumiaje elimu uliyonayo ? je unaigeuza vipi ili iwe Biashara? Usidharau mwanzo wa vitu vidogo maana katika udogo ndio vitu vinakuwa vikubwa. 5.KITU UNACHOKIPENDA SANA (Passion) Ngazi ya tano ni kufuata kitu unachokipenda sana, Kitu unachokipenda sana kinaweza kikakufanya wewe kufurahia kile kitu hata ukawa tayari kukutana na vikwazo na kuvikabili halafu uko tayari hata kusonga mbele hata kama utakutana na matatizo mengi, mfano mimi leo niliyoyafanya katika kuandika vitabu, sio kwamba huko nyuma kote nilikuwa napata mrejesho wa kifedha kwa haya mambo hapana, ilinichukua miaka mingi sana kabla sijaona mrejesho wa kifedha, miaka kadhaa ya nyuma nilikuwa naenda kufanya semina mahali wanakuja watu wachache naandika vitabu wananunua watu watano au kumi,yote haya yalikuwa yanatokea lakini hayakuwa yananikatisha tamaa kwa sababu ya passion hata nikikatishwa tamaa nilikuwa nasonga mbele. 6.JINSI ULIVYO Pointi ya tano na nusu ni Jinsi ulivyo, wakati mwingine jinsi mtu alivyo inaweza ikawa ni njia mojawapo ya kugundua yeye anatakiwa afanye nini, kwa mfano mtu kama Joti unatamani tu ucheke jinsi alivyo alivyo au Hasheem Thabiti bonge la mtu futi 7 nukta kadhaa, labda wewe ni baunsa huenda kuna shughuli unatakiwa kuifanya, Hivyo katika hayo mambo matano hapo juu nimesema kwanza kabisa Angalia kipaji ulichonacho, Pili Angalia uzoefu ulionao., tatu Uwezo uliojijengea, nne ni Elimu na tano ni yale uyapendayo sana na tano na nusu ni Jinsi ulivyo. HITIMISHO MASWALI 1. Je utafanya biashara kwa kutumia kigezo gani? 2 Je hofu yako ni nini ? 3. Utahitaji sapoti ya watu gani ili uanze bila fedha? 4. Je utajitangaza vipi ili uweze kupata wateja? 5. Je ungependa ufike wapi kwa kuchagua mlango/ kipengele kimojawapo?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

picha